Mara
ya mwisho kukutana timu hizi katika ardhi ya Tanzania, ilikuwa ni mwaka
1996, katika michuano hii ya Kagame. Takribani miaka 19 imepita kabla
ya kuwakutanisha tena hapo kesho.
Yanga.
Wachezaji wa kutazamwa.
Wachezaji watakaoleta raha kuwatazama ni Donald Ngoma, Niyonzima, Msuva, Canavaro na Amis Tambwe.
Mafanikio.
Yanga imefanikiwa kutwaa taji hilo mara 5 (mwaka 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012).
Gor Mahia.
Wachezaji wa kutazamwa.
Wachezaji watakaoleta raha kuwatazama ni Michael Olunga, Meddie Kagere, Boniface Olouch, George Odhiambo na Godfrey Watusumbi.
Mafanikio.
Mabingwa mara 5 wa michuano hiyo (mwaka 1976, 1977, 1980, 1981 na 1985).
Hii
ni fainali kabla hata fainali haijafikia, Yanga wanatamba kwa kuwa na
kikosi bora. Falsafa yao kwa sasa ni soka la kushambulia mwanzo hadi
mwisho.
Gor Mahia hawapo nyuma hakuna asiyefahamu timu za Kenya zinapokutana na za Tanzania nini hutokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni