Timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, jana imetaja wachezaji wake wapya nane iliyowasijili, Uhuru akiwa miongoni mwao.
Mwenyekiti wa Ezenkosi na kocha Mkuu wa timu hiyo, Jomo Sono amewaambia Waandishi wa Habari jana mjini Sandton, Johannesburg kwamba sasa wako tayari kwa LIgi Kuu ya ABSA.
“Tumesajili wachezaji Fulani wazuri sana,”amesema Somo, ambaye ndiye mmiliki
Uhuru ambaye msimu uliopita alitolewa kwa mkopo Simba SC kwenda Mwadui FC iliyokuwa Daraja la Kwanza na akafanikiwa kuipandisha Ligi Kuu, amesema kwamba kutua kwake Cosmo ni matunda ya kutokata tamaa na kupambana ili kutimiza ndoto.
“Nimefurahi kujiunga na Cosmos, hii ni fursa nyingine kwangu kuonyesha uwezo wangu na kufufua ndoto ambazo zilianza kufifia kutokana na matatizo ya hapa na pale, wakati nacheza nyumbani,”amesema mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union na Azam FC.
Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Cosmos, ni Mohammad Sulumba kutoka Blantyre United, Miciam Mhone kutoka Blue Eagles zote za Malawi, Sibusiso Mdamba kutoka African Warriors, Pako Mahaabo kutoka Chuo cha Maluti FET, Michael Gumede kutoka Thanda Royal Zulu, Conrad Madolo kutoka Garankuwa United na Mxolisi Macuphu kutoka Royal Eagles.
Sasa katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu huu kutakuwa na Watanzania, wawili baada ya Mrisho Khalfan Ngassa kusaini Mkataba wa miaka minne Free State Stars Mei mwaka huu akitokea Yanga SC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni