TIMU
ya Manchester United imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England baada
ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Newcastle United Uwanja wa Old
Trafford mchana wa leo.
Nahodha
wa Manchester United, Wayne Rooney alimtungua kipa Tim Krul kuifungia
timu yake kipindi cha kwanza, lakini akanyooshewa kibendera cha kuotea.
Kikosi
cha Manchester United kilikuwa; Romero, Darmian/Valencia dk77,
Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Schweinsteiger/Carrick dk59, Mata,
Januzaj/Hernandez dk67, Depay na Rooney.
Newcastle
United: Krul, Coloccini, Mbemba, Taylor, Haidara, Anita, Colback,
Obertan/Thauvin dk69, Wijnaldum, Perez/Tiote dk78 na Mitrovic/Cisse
dk88.
Rooney akiwa kajifunika uso baada ya mwamuzi kukataa goli lake
Golikipa wa Newcastle Krul denies akiokoa mkwaju wa Javier Hernandez.
Ed Woodward alie rejea kutoka nchini Hispania baada ya kushindwa kumsajili Pedro alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Manchester United walio hudhuria mtanange


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni