
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa gazeti la michezo nchini Italia la Gazzetta dello sport aitwaye Emanuele Giulianelli.
Mwandishi huyo anaamini Benzema atafanyiwa vipimo vya afya mapema siku ya jumatatu kabla ya kutambulishwa usiku mbele ya mashabiki wa Arsenal kwenye mchezo dhidi ya Liverpool
Giulianelli ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa "Arsenal wamekodi ndege binafsi itakayo safiri kwenda kumchukua Benzema siku ya Jumapili jioni"
"Atafanya vipimo jumatatu mchana kabla ya kutambulishwa baadae kwenye mchezo dhidi ya Liverpool" alimaliza Giulianelli.
Taarifa hii imekuja baada ya siku moja kupita ambapo mshambuliaji wa zamani wa Qpr na Fulham Rodney Marsh kudai kuwa Real Madrid wamekubali kumuuza Benzema kwenda Arsenal kwa ada inayodhaniwa kuwa ni paundi milioni 48.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni