Si ulisikia ile ishu ya yule dogo mwenye miaka mitano aliyelipiwa usafiri yeye
na familia yake na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ili akamuone straika Robin
van Persie ambaye alimwaga chozi baada ya kusikia amehama Man United?
Louis Diamond ni shabiki mkubwa wa Man United, lakini leo
akiwa na wadogo zake amevaa jezi ya Fernabahce na kukutana na shujaa wake.
Ilikuwa furaha ya aina yake wakati alipojumuika live na van
Persie ambaye alimliza kwa uchungu ile mbaya.
Diamond pia alipata nafasi ya kumuona van Persie akiitumikia
Fenerbahce ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kati Ligi Kuu ya Uturuki dhidi ya Eskisehirspor.
Diamond sasa moyo mweupee na yu tayari kurejea Engaland sasa.
ALIPOWASILI AKIWA NA WAZAZI WAKE |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni