Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa Tenisi Novak
Djokovic jana alilalama kwa msimamizi wa mchezo kwamba alikuwa akinusa harufu
ya bangi katika ukumbi wa mechi ya kombe la Rodgers aliomshinda Jemery Chardy.
Baada
ya kushinda seti ya kwanza ,raia huyo wa Serbia alimfuata msimamizi wa mechi
hiyo na kusema kuwa, ''Kuna mtu anavuta bangi ,naweza kunusa harufu yake na
nasikia kizunguzungu''.
Baadaye
Djokovic aliwaambia maripota:''Huwezi kuamini ilivyokuwa ikiniathiri,yeyote
ambaye alikuwa akivuta,natumai hatarudi tena kesho,nadhani amejificha katika
mbingu ya saba''.
Djokovic
alisema kuwa alinusa harufu hiyo wakati wa mechi yake ya wachezaji wawili kila
upande na mwenzake Janko Tipsarevic siku ya ijumaa.
''Jana
nilinusa katika mechi ya wachezaji wawili kila upande ,leo tena. Lazima kuna
mtu ambaye anajivinjari katika ukumbi huu” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni