JIJI la Beijing limechaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki na Paralimpiki ya majira ya baridi wakiushinda mji wa Almaty ulioko Kazakhstan.
Wakiwa wenyeji wa michuano ya olimpiki mwaka 2008, Beijing ambao ndio mji kuu wa China sasa unakuwa mji wa kwanza kuandaa michuano yote miwili ya majira ya kiangazi na baridi.
Miji ya Beijing na Almaty haikuwa ikipewa nafasi wakati kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo kilipoanza miaka miwili iliyopita.
Lakini baada ya miji kadhaa ya Ulaya kujitoa kutokana na sababu za kisiasa au kiuchumi, Beijing ilifanikiwa kuibuka kidedea kwa kuzoa kura 44 dhidi ya kura 40 za Almaty.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni