Tottenham imetangaza kumsajili Mcameroon Clinton N'Jie kutoka Lyon kwa ada ya Pauni Milioni 10
WASIFU WA CLINTON N'JIE
Kuzaliwa: Agosti 15, 1993
Ameicheza mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita
Alijiunga
na Lyon mwaka 2010 kwa msaada wa kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo,
Jean-Jacques Nono. Novemba 2012 aliichezea mechi ya kwanza Lyon akitokea
benchi timu ikishinda 3-0 dhidi ya Reims, kabla ya msimu uliopita
kung'ara katika Ligue 1, akifunga mabao nane katika mechi 33 za
mashindano yote 15 tu akianza.
KLABU
ya Tottenham Hotspur ya Ligi Kuu ya England imethibitisha kumsajili
mwanasoka wa kimataifa wa Cameroon, Clinton N'Jie kutoka klabu ya Lyon
ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 ambayo italipwa baada ya kuruhusiwa kucheza.
Mshambuliaji
huyo chipukizi wa Simba Wasiofungika, atalipwa Pauni Milioni 1.5 baada
ya kusaini Mkataba wa miaka mitano na klabu ya White Hart Lane.
Kocha
wa Spurs, Mauricio Pochettino amelazimika kuongeza watu katika safu
yake ya ushambuliaji ili kuiongezea makali kabla ya dirisha kufungwa
Septemba 1, mwaka huu.
Na N'Jie anatarajiwa kuisaidia sana Spurs kutokana na umahiri wake katika safu ya ushambuliaji.
Kinda huyo aliyezaliwa Agosti 15, mwaka 1993 hadi sasa tayari ameichezea mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita. Alijiunga na Lyon mwaka 2010, baada ya kusukiwa mipango na kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo, Jean-Jacques Nono.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni