Gazeti la The Sun limekamilisha
udaku wake na leo limekuja na kichwa cha habari kikisema kwamba daktari
wa Chelsea, Eva Carneiro anawatumia vibaya wachezaji wa klabu hiyo.
Stori
hii imekuja wiki ya kwanza tu baada ya Carneiro kushambuliwa hadharani
na kocha Jose Mourinho kufuatia kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard
wakati wa dakika za mwisho za mechi ambayo Chelsea walitoka sare ya 2-2
na Swansea City.
Matokeo yake, Carneiro amepunguziwa majukumu katika benchi la matabibu la Chelsea.
The Sun wamemshambulia Daktari huyo mwenye heshima kubwa kuwa ana mahusiano ya mapenzi na baadhi ya wachezaji wa Chelsea.
Mpenzi wa zamani wa Eva, Rupert
Patterson-Ward, ndiye amevujisha taarifa hiyo kwa gazeti hilo akidai
kwamba daktari huyo analala na moja ya wachezaji wa klabu hiyo, ingawa
hajataja jina lake.
Nukuu hii hapa:
"Mwanamke
huyu aliharibu maisha yangu. Eva angeweza kuniambi kwamba analala na
moja ya wachezaji wa Chelsea, lakini alijua ningejisikia vibaya. Pia
huenda alidhani siwezi kuamini.
Eva anajivunia sana kuwa maarufu miongoni mwa wachezaji. Anapenda sana kusifiwa".
"Eva
ni mwanamke mwenye mvuto na watu wengi hawajui. Ana ushawishi mkubwa,
anaweza kupata kila anachohitaji. Nilikaa naye katika mahusiano na
tulipanga kuwa na familia, lakini aliniumiza na kunimwaga".
"Eva anapenda sana kufanya mapenzi. Mapenzi ni muhimu sana kwake. Tulikuwa tunafanya mapenzi kila siku".
Sio kwamba Rupert
Patterson-Ward amewapa tu stori hiyo ya aibu, jamaa amevujisha mpaka
picha zinazothibitisha kwamba wawili hao walikuwa wapenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni