De Gea anataka kutimka Man United na kujiunga Real Madrid
Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amesema kitendo cha David De Gea kutaka kuondoka Old Trafford ni kwasababu ya utawala mbovu wa klabu hiyo.
Bosi
wa Mashetani Wekundu, Louis van Gaal amedai golikipa huyo hataki
kukichezea tena kikosi chake, ingawa De Gea ameshitushwa na kitendo cha
kutopangwa kwenye timu hiyo ya Mholanzi.
Akizungumza
na Sky Sports News, Neville amesisitiza kwamba hali hiyo imetokea
kwasababu ya uzembe wa utawala wa Man United wa kuacha mkataba wa kipa
huyo wa Hispania kufikia mwaka wa mwisho.
"Mwazoni
alikuwa na msimu mbaya, hakuwa na uzoefu wowote, akaendelea kuzoea
mazingira ya England, chini ya David Moyes alionesa thamani yake".
"Swali
la kujiuliza, kwanini mkataba wake haukuongezwa siku za nyuma? kumuacha
abakize mwaka mmoja ni utawala mbovu. Sasa United wanalimaliza vipi? "
Ameuliza nyota huyo wa zamani mwenye miaka 40 kwasasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni