Mshambuliaji
raia wa Senegal Papa Niang ameshawasili jijini Dar es Salaam leo
taayari kwa ajili ya kuanza majaribio yake ya kujiunga na klabu ya
‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba SC.
Niang
leo ataunganishwa moja kwa moja na kikosi cha Simba ambacho kitafanya
mazoezi yake kwenye uwanja wa Boko ambako ndipo kikosi hicho kinafanya
mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara
inayotarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu.
Katika
majaribio yake, endapo Niang ataonesha kiwango cha kumvutia kocha mkuu
wa Simba Dylan Kerr pamoja na benchi zima la ufundi la kikosi hicho,
basi huenda akapewa mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ambayo imekuwa
ikihaha kutafuta washambuliaji wa kigeni.
Hivi
karibuni Simba ilimleta mshambuliaji wa kigeni kutoka Burundi Kelvin
Ndayisenga ambaye alicheza kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi
ya URA FC ya Uganda huku akifanikiwa kuifungia timu hiyo goli moja
kwenye ushindi wa goli 2-1.
Inasemekana
Simba imeachana na mshambuliaji huyo baada ya kushindwa kufikia
makubaliano katika masuala ya pesa ambapo Ndayisenga alitaka dau kubwa
Simba wakashindwa kufikia na kuamua kumruhusu aondoke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni