Kocha
mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa ametoa orodha ya wachezaji 22
watakaosafiri usiku wa jumapili kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya
wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria Septemba 05, 2015.
Orodha
hiyo ya wachezaji 22 imetoka katika kikosi kilichotangazwa wiki mbili
zilizopita na kocha mkuu wa Taifa Stars, ambapo walipata nafasi ya
kufanya mazoezi kwa takribani wiki moja katika uwanja wa Karume.
Wachezaji
wote waliochaguliwa timu ya Taifa wanapaswa kuripoti kambini Tansoma
Hoteli siku ya jumapili saa 5 asubuhi kwa maandalizi ya mwisho ya safari
hiyo.
Wachezaji
waliochaguliwa ni All Mustafa (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Said
Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam FC), Abdi Banda,
Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba SC), Juma Abdul, Haji Mngwali,
Kelvin Yondani, Nadir Haroub (Yanga SC).
Viungo
Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deus
Kaseke (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Washambuliaji John Bocco,
Farid Musa, (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Saimon Msuva (Yanga
SC), na Ibrahim Ajib (Simba SC).
Taifa
Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku kwa usafiri wa shirika la
ndege la Uturuki (Turkish Airlines), na kufika jumatatu asubuhi jijini
Istanbul, ambapo timu itaelekea katika mji wa Kocael ambapo itaweka
kambi ya wiki moja katika hoteli ya Green Park Kartepe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni