Boniface Wambura, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi
Dirisha
la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) limefungwa jana ambapo vilabu vitatu
tu vya VPL vimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji katika muda
uliopangwa.
Klabu
za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya
jijini Mwanza zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji, faini
ni laki tano (500,000) kwa kila klabu iliyochelewesha usajili au
itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya tarehe ya jana.
Awali
TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini kukamilisha
usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya
wakati, vilabu 24 vya ligi daraja la kwanza, vilabu 24 ligi daraja la
pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni