
Meneja
wa Manchester United Van Gaal amesema kwamba hana haja ya kuimarisha
washambuliaji wake baada ya timu yake kutoka sare 1-1 na Newcastle
Mshambuliaji Wayne Rooney hajafanikiwa kuona wavu kutoka tarehe 4 mwezi Aprili
United ilikuwa na matumaini ya kumsajili Pedro, kabla ya mshambualiaji huyo kundoka Barcelona na kujiunga na wapinzani wao sugu Chelsea.
Alipoulizwa kama alihitaji kusajili washambualiaji alisema
United walikosa nafasi tele kuchukua uongozi dhidi ya Newcastle, Bao la Rooney lilikatiliwa baada ya kupatikana kaotea huku jaribio la Chris Smalling kwa kichwa likiambulia patupu baada ya kugonga mwamba.
"Wayne alifunga ni vile tu haikuruhusiwa," aliongeza Van Gaal.
"Lakini pia ni mpira wa miguu nilivyosema mara nyingi unahitaji vifaa zaidi ili kusaidia uamuzi wa refariii."
"Wasiwasi ni kwamba lazima tutawale mpinzani wetu, na hivyo ndivyo tulifanya leo na pia dhidi ya Aston Villa, Tottenham and Brugge, nimetosheka na vile walivyocheza leo na si matokeo".



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni