Nyota wa zamani wa Arsenal Thiery Henry anaimani kubwa kwamba huu
ni msimu ambao Arsenal wanapaswa kutwaa ‘ndoo’ ya EPL na kumaliza ukame
wa miaka takriban 11 ya ubingwa wa EPL.
Miamba hao wa London Kaskazini kwa sasa wanashika nafasi ya pili
katika msimamo wa EPL nyuma ya Manchester City lakini wakitofautiana kwa
idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga wakishinda michezo yao yote
minne ya mwisho ya ligi.
Vijana hao wa Arsene Wenger wameshinda michezo yao minne kwa
ushindi wa kishindo dhidi ya Leicester City, Manchester United na
Watford, wakati huo huo wakiwafunga mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich
katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya huku wakionesha soka la
ushindani wa hali ya juu katika siku za hivi karibuni hasa katika mechi
zenye ushindani mkubwa.
Akiongea na TalkSPORT
Jumanne wiki hii, Henry aliongea kwa kujiamini kuhusu timu yake hiyo ya
zamani kunyakua ubingwa, akisema: ‘Nasema kwa dhati kabisa huu ni mwaka
wao.
Wanapata matokeo dhidi ya timu kubwa sasa na matokeo hayo yanawapa
nguvu kubwa ya kujiamini. Hilo ndio jambo kubwa’.
Viwango bora vya Olivier Giroud na Theo Walcott ni mchango mkubwa
sana kwa matokeo mazuri ya Arsenal katika siku za karibuni huku
washambulizi hao wakionekana kuchuana vikali hali inayoongeza ushindani
katika safu ya ushambuliaji miongoni mwao.
‘Theo Walcott kucheza kama mshambuliaji wa kati kunamsukuma Giroud aongeze juhudi, na vivyo hivyo kwa Giroud.’
Henry pia amewapongeza Mesut Ozil, Santi Cazorla Hector Bellerin na
Petr Cech kwa viwango vyao bora ambavyo ndio mchango mkubwa kwa matokeo
mazuri ya klabu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni