Baada ya klabu ya FC Barcelona kuchukua kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Sevilla siku ya Jumamosi ya October 3 katika uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan, wapinzani wao wa jadi Real Madrid waliingia dimbani Jumapili ya October 4 katika uwanja wa ugenini wa Estadio Vicente Calderon kucheza mechi na wapinzani wao kutoka mji mmoja wa Madrid.
Real Madrid waliingia kucheza mechi dhidi ya wenyeji wao Atletico Madrid, kwa kawaida FC Barcelona na Real Madrid huwa wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa Atletico Madrid kila mara wakutanapo, licha ya Real Madrid kuanza kwa kupachika goli la mapema kupitia kwa Karim Benzema dakika ya 9′ .
Goli ambalo halikuweza kuipatia ushindi na kuondoka na point 3 katika uwanja wa Estadio Vicente Calderon, kwani Atletico Madrid walikuja juu dakika ya 22 ya mchezo wakapata penati na Antoine Griezmann kukosa, ila hiyo ilikuwa kama chachu kwa Atletico Madrid kuendelea kutafuta nafasi, kwani kipindi cha pili dakika ya 83 Luciano Dario Vietto akaisawazishia Atletico Madrid na kufanya mechi kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni