Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amesema kamwe hatakimbia Stamford
Bridge eti kisa kile kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Southampton.
Lakini akasisitiza, kama wanataka kumfukuza, poa tu lakini
watajuta kumfukuza kocha gwiji ambaye hawakuwahi kuwa naye.
Mourinho ameiambia runinga ya Sky hivi: “Moja, kamwe siwezi
kukimbia, siwezi kukimbia majukumu yangu.”
“Pili kama klabu wanataka kunitimua, basi wafanye hivyo lakini
watajuta kumfukuza kocha bora kama mimi.”
Licha ya kutangulia kufunga, Chelsea ikiwa nyumbani
imekutana na kipigo hicho cha mabao 3-1 dhidi ya Southampton.
BOSI ANAANGALIA TU... |
MOURINHO ANACHANGANYIKIWA.... |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni