STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 2 Oktoba 2015

STARS YAANZA KUJIFUA KUIVAA MALAWI...........

Stars Mazoezi Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo mchana katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo dhdi ya Malawi utakaochezwa Jumatano Oktoba 7, 2015 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Stars inayonolewa na kocha mkuu mzawa Charles Mkwasa, akisaidiwa na Hemed Morocco, Peter Manyika na mshauri wa Ufundi Abdallah Kibadeni wameingia kambini jana katika hoteli ya Urban Rose iliyopo Kisutu jijini Dar es salaam.

Wachezaji wote wameripoti kambini isipokuwa wachezaji wa kimataifa wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaotarajiwa kuungana na wenzao mwishoni mwa wiki baada ya kumaliza michezo inayowakabili wikiendi hii.

Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa: All Mustafa, Aishi Manula, na Said Mohamed.

Walinzi: Juma Abdul, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Haji Mwinyi, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wengine ni viungo: Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa.

Washambuliaji: John Bocco, Rashid Mandawa na Ibrahim Hajibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox