Petr Cech amefichua kwamba anataka
kuanza kucheza bila ya kuvaa helmet kichwani mwake lakini amekutana na upinzani
mkali toka kwa madaktari wake.
Mlinda mlango huyo wa zamani wa
Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga na Arsenal amekuwa akivaa helmet tangu mwaka
2006 baada ya kupata mpasuko katika fuvu la kichwa chake kufuatia kugongana na
kiungo wa Reading Nicky Hunt tukio lililofanya awe nje ya uwanja kwa kipindi
kirefu.
Cech , 33,amesema kuwa amechoka kuvaa helmet
akidai kuwa inampunguzia kujiamini na hata kufanya mawasiliano kati yake na
wachezaji wenzake uwanjani kuwa magumu kutokana na masikio yake kuwa yamezibwa.
Amesema "Ningekuwa najiamini sana kama
nisingekuwa navaa helmet.Kama unapenda ama hupendi,helmet inaathiri sana
mazingira yangu.Madaktari wameniambia niendelee kuvaa ili niendelee kuwa
salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni