Kiungo wa Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas ameelezea hasira kutokana na matokeo duni ya klabu ya Chelsea msimu huu.
Mabingwa hao watetezi wameshindwa mechi 7 kati ya 12 walizocheza msimu hu.
The Blues' wana alama tatu tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja.
'Sijui nini kinaendelea ,,,tumekuwa tukicheza vyema ila hatuna bahati ya kufunga bao' alisema kiungo huyo wa kati.
'Kwa wakati mwengine,huwa ukidana mpira na uguse kidogo unapaa na kuingia ,lakini hivi sasa hata ukifuma mkwaju unakwenda nje' Fabregas aliiambia Gazeti la kihispania Marca.
'Tunahitaji kuanza kushinda mechi zetu kwa udi na uvumba la sivyo haitukuwa vyema'
Kiungo hicho cha kati cha timu ya Uhispania ni mmoja kati ya wale wanaolaumiwa na kocha Jose Mourinho kukuzembea msimu huu.
Majuma mawili yaliyopita Fabregas alikanusha kuwa wachezaji wanafanya mgomo baridi dhidi ya kocha wa Chelsea Mourinho.
Fabregas alisema kuwa anafurahia sana uhusiano wake na meneja huyo mbishi mbali na muda wake akiwa London.
London,England.
Petr Cech amefichua kwamba anataka kuanza kucheza bila ya kuvaa helmet
kichwani mwake lakini amekutana na upinzani mkali toka kwa madaktari
wake.
Mlinda mlango huyo wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga na
Arsenal amekuwa akivaa helmet tangu mwaka 2006 baada ya kupata mpasuko
katika fuvu la kichwa chake kufuatia kugongana na kiungo wa Reading
Nicky Hunt tukio lililofanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Cech , 33,amesema kuwa amechoka kuvaa helmet akidai kuwa inampunguzia
kujiamini na hata kufanya mawasiliano kati yake na wachezaji wenzake
uwanjani kuwa magumu kutokana na masikio yake kuwa yamezibwa.
Amesema "Ningekuwa najiamini sana kama nisingekuwa navaa helmet.Kama
unapenda ama hupendi,helmet inaathiri sana mazingira yangu.Madaktari
wameniambia niendelee kuvaa ili niendelee kuwa salama.
Wakati huo huo Cech amekiri kuwa uvaaji wa helmet umemsaidia kwani
ameshakutana na matukio mengine mawili ya kugongwa kichwani lakini
akabaki salama.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni