MSHAMBULIAJI wa
kimataifa wa Uholanzi, Dick Kuyt amebainisha alikuwepo Disneyland Paris
muda huohuo ambao magaidi walishambulia viunga kadhaa vya mji mkuu huo
wa Ufaransa.
Zaidi ya watu 120 waliuawa na wengine 99 kuachwa katika
hali mbaya Ijumaa iliyopita, huku Uwanja wa Stade de France ambao timu
ya taifa ya nchi hiyo ilikuw ikicheza na Ujerumani mchezo wa kirafiki
ikiwa moja ya maeneo yaliyoshambuliwa.
Wakati wa matukio hayo
yakiendelea Kuyt ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Feyenoord
alikuwa na familia yake wakiendelea kufurahia mapumziko yao huko
Disney.
Akihojiwa Kuyt amesema watu wake wengi wa karibu walikuwa
wakifahamu kuwa yuko Paris hivyo baada ya kusikia tukio hilo walitafuta
kupitia simu yangu lakini haikupatikana kwasababu alikuwa
ameizima.
Lakini baadae kwa kutumia simu ya mke wake aliwafahamu watu
wake wote wa karibu kuwa yuko salama wasihofu.
Kuyt aliendelea kudai
kuwa eneo alilokuwepo ilikuwa ni kilometa 20 kutoka mahali mashambulio
yalipofanyika hivyo hakupata wasaa wa kujua ukubwa wa tatizo mpaka
aliporejea hotelini na kuona taarifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni