STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 16 Novemba 2015

MESSI AANZA MAZOEZI NA KIKOSI B.................


MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameanza kufanya mazoezi katika timu B na anaonekana anakaribia kupona kabisa.
 
 Kocha wa timu B, Gerard Lopez amesema kumekuwa dalili njema kutoka Messi ambaye amekuwa nje ya uwanja toka alipoumia goti katika mchezo dhidi ya Las Palmas Septemba 26 mwaka huu. 
 
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina anategemewa kuukosa mchezo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao Real Madrid Jumamosi hii kwasababu ya majeruhi lakini Lopez amebainisha Messi amekuwa akifanya mazoezi na kikosi chake na kuonyesha maendeleo mazuri.
 
 Lopez amesema Messi alikamilisha mazoezi na alionekana kutokuwa na tatizo lolote hivyo anadhani hizo ni dalili njema.
 
 Lopez aliendelea kudai kuwa anashukuru kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 kufanya nao mazoezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox