Jana ilikua ni siku ya kipekee kwa mashabiki wa soka waliokuwa wamefurika katika uwanja wa Old Trafford mjini Manchester pale waliposhuhudia malegendari wa zamani wakimenyana katika mchezo wa kuchangia watoto ulioandaliwa na shirika la watoto ulimwenguni UNICEF.
Katika mchezo huo uliozikutanisha timu mbili, moja ikiwa chini ya David Beckham na kocha wake Sir Alex Ferguson wakijumuisha wachezaji wenye asili ya kiingereza na timu nyingine ilikua chini ya Carlos Figo na kocha wake Carlo Ancelotti wakiwakilisha wachezaji kutoka sehemu nyingine ya dunia.
Katika mchezo huo magoli yaliyofungwa na Paul Scholes na Michael Owen (2) yalitosha kuipa ushindi timu ya Beckham kwa magoli 3 dhidi ya moja lililofungwa na Dwight Yorke wa kikosi cha akina Figo na Ronaldinho.
David Beckham alitoka dakika 16 za mwisho na kubadiliwa na mwanae Brooklin Beckham mwenye miaka 16 katika tukio lililovuta hisia za watu wengi huku Becks akirudi tena kuungana na mwanae baada ya Sol Campbell kuumia dakika za lala salama.
Bahati mbaya katika mchezo huu ilikua ni kukosekana kwa Zinedine Zidane ‘Zizzou’ pamoja na Patrick Viera ambapo Beckham alisema ilikua ni ngumu kwa Zizou kuja kutokana na msiba mkubwa uliotokea jijini Paris Ufaransa juzi usiku kutokana na shambulio la kigaidi na kuua watu zaidi ya 128.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni