
Ribery amefungua kesi hiyo baada ya kituo hicho cha TV kutumia picha ya mwanasoka huyo katika kuelezea story juu ya matibabu ya cryotherapy – matibabu yanayohusisha kuuweka mwili kwenye sehemu kavu au yenye baridi kali ili kupunguza maumivu au kuponyesha kabisa.
“Mr Franck Ribéry … hakutoa ruhusa ya matumizi ya picha ile kwa kituo cha CNN,” alisema Carlo Alberto Busa ambaye ni mwanasheria wa Ribery wakati akiongea na radio ya Ufaransa – RMC
Picha hiyo ya Ribery ilionekana kwenye akaunti ya Twitter ya CNN na Ribery alionekana kwenye box la cryotherapy huku picha ikisindikizwa na kichwa cha habari kifuatacho: “Mwanamke hakutwa ameganda kwenye box la cryotherapy, matibabu haya yazua maswali.”
Busa
aliongeza: “Mr Franck Ribéry na familia yake wamenielekeza niende
kwenye mahakama nchini Ufaransa kufungua kesi ya kudai fidia isiyopungua
$1.5m”


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni