David Moyes
amefutwa kazi kama meneja wa klabu ya Real Sociedad ya Uhispania, siku
moja kabla yake kuadhimisha mwaka mmoja katika klabu hiyo.
Lakini klabu hiyo sasa imo karibu sana na eneo la kushushwa daraja, ikiwa juu pekee kutokana na wingi wa mabao baada ya kulazwa 2-0 Ijumaa ugenini Las Palmas, ikiwa mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano ligini.
Taarifa kutoka kwa Sociedad imesema klabu hiyo imeamua kukatiza mkataba wa Moyes.
Meneja msaidizi Billy McKinlay pia amefutwa kazi.Klabu hiyo kwa sasa imo nambari 16 ligini na itakutana na washindi wa Europa League Sevilla na mabingwa wa Ulaya Barcelona mechi mbili zijazo La Liga baada ya mapumziko ya kimataifa.
Kibarua hicho Sociedad kilikuwa cha kwanza kwa Moyes kupata baada ya kufutwa kama meneja wa Manchester United Aprili 2014 baada ya kuwaongoza kwa miezi 10 pekee.
Moyes, aliyekaa miaka 11 Everton kabla ya kumrithi Sir Alex Ferguson Old Trafford, alitia saini mkataba ambao ungemuweka Uhispania hadi Juni 2016 na alikuwa meneja wa nne Mwingereza kuinoa Sociedad.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni