MENEJA wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ataongoza Kikosi cha Timu ya Great Britain and Ireland XI ambacho Kepteni wake atakuwa David Beckham kwenye Mechi ya Hisani siku ya leo jumamosi.
Timu hiyo ya Uingereza na Ireland itapambana na Kikosi cha Dunia ambacho Nahodha wake atakuwa Lejendari wa Ufaransa Zinedine Zidane chini ya Meneja Carlo Ancelotti.
Refa wa Mechi hiyo itakayochezwa leo Uwanja wa Old Trafford Jijijni Manchester ni Nguli wa Italy Pierluigi Collina.
Mechi hii ya Hisani ni kwa ajili ya kuchangisha Fedha kwa ajili ya Mfuko wa Shirikisho la Umoja wa Mataifa la Kusaidia Watoto, UNICEF.
Beckham akiwa South America nchini Argetina, Buenos Aeries
Ferguson, mwenye Miaka 73, alistaafu Soka Mwaka 2013, baada ya kutwaa Makombe 38 katika Miaka yake 26 huko old Trafford akiwa Meneja wa Man United.
Beckham, ambae pia alikuwa Nahodha wa England, aliichezea Man United Mechi 394 kwa Miaka 11 kabla kuhamia Real Madrid Mwaka 2003.
Akiongelea Mechii hii, Beckham, mwenye Miaka 40, alisema:
“Kila Mtu anajua nilistaafu Miaka Mitatu ilitopita na sikutegemea kama nitavaa Viatu tena na kucheza. Lakini Soka ina mvuto mkubwa na kuwa na Zidane Uwanjani, Sir Alex Ferguson na Carlo Ancelotti pembeni, nadhani Watu watafurahia.”
Beckham, ambae ni Balozi Maalum wa UNICEF, aliongeza: “Mechi hii ni mahsusi kuleta mwamko na kuchangisha Fedha kusaidia Watoto wenye kuhitaji msaada.”
David Beckham (kulia) na Zinedine Zidane (kushoto) 2005- Bernabeu
Ryan Gigs (nyuma) na Beckham (mbele) wakishangilia baada ya Beckam kufunga dhidi ya Leicester
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni