Hali si shwari jijini Paris, Ufaransa mara baada ya magaidi kufanya mashambulio makubwa mawili ya risasi na moja la bomu karibu na uwanja uliokuwa unachezewa mechi kati ya timu ya taifa ya Ufaransa na Ujerumani, Stade de France usiku wa kuamkia leo.
Magaidi hao walifanya mashambulizi katika ukumbi mmoja wa starehe ‘Concert Hall’ na kuua watu wasiopungua 149 hadi hivi sasa kabla ya polisi kuwakabili.
Hali hiyo ilileta hofu kubwa kiwanjani baada ya milio mikubwa ya makombora kusikika wakati wachezaji wakiwa wanacheza mpira huku raisi wa nchi (Ufaransa) akiwa nae uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki.
Oliver Giroud aliifungia goli Ufaransa na kuipa ushindi timu yake wa magoli 2-0 dhidi ya ujerumani ambayo kocha wake Joachim Low ametaja hofu kubwa miongoni mwa timu yao ilipunguza morali mara baada ya mabomu kusikika karibu na hoteli yao.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande (kushoto) akiwasiliana na maafisa wa usalama uwanjani Stade de France
Taarifa zinasema huenda kusiwepo na mechi ya kirafiki Jumanne hii kati ya England na Ufaransa iliyopangwa kufanyika katika uwanja wa Wembley jijini London.
Vyama vya soka vya FA na FFF vitatoa ripoti hivi karibuni kuhusiana na hilo.
Hali si shwari, rais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari nchini humo huku mipaka ikifungwa na jeshi linaendelea na kazi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni