Polisi wamelazimika kuwatoa wachezaji wa timu ya
taifa Ujerumani mjini Paris, Ufaransa baada ya kuwepo kwa taarifa ya bomu.
Taarifa hizo zilitolewa na mtu mmoja aliyejiita
raia mwema akidai kuna bomu eneo hilo.
Ilikuwa ni saa 3:50 asubuhi, Polisi wa Ufaransa
walipolazimika kufika hotelini hapo na kuwaondoa wachezaji hao wa timu ya taifa
ya Ujerumani walio mjini hapo kujiandaa na mechi yao kirafiki dhidi ya wenyeji
Ufaransa, leo.
Hata hivyo uchunguzi wa mwisho wa polisi baadaye
ulibaini eneo hilo lilikuwa salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni