Ronaldo amesema hatomtaja mama wa mtoto wake mpaka atakapoona muda umefikaMchezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, amesema kamwe hatomtaja
mama mzazi wa mtoto wake Ronaldo Jr. na kwamba muda ukifika atamuweka
wazi huku mwanae pia akitakiwa kusubiri muda muafaka apate kumjua mama
yake.
Amesema kuwa amekua akishiriki mapenzi na warembo tofauti tofauti
huku akikiri kuwa hiyo sio yeye tu bali ni tatizo kwa nyota wengi
duniani kupitia maisha hayo huku akijinasibu kuwa kwasababu yeye ni
mrefu, mwenye mwili mzuri wa mazoezi basi huwamaliza akina dada. Ronaldo ameweka wazi maisha yake binafsi wakati akifanyiwa mahojiano na Jonathan RossKuhusu Balon d’Or msimu huu, Ronaldo anasema Messi atatwaa tuzo hiyo
kutokana na klabu yake ya Barcelona kutwaa makombe yote matatu
iliyoshiriki msimu uliopita. Huku Ronaldo akisema ulikua ni msimu mzuri
zaidi kwake binafsi kutokana na kufunga magoli mengi katika kila
mashindano.
Ronaldo ambaye alikua jijini London kwa utambulisho wa filamu yake ya
maisha yake ya soka, anasema kamwe hatarajii kustaafu hivi karibuni
huku akisema atamaliza mpira wake katika ligi bora na sio Marekani wala
Qatar. Huku akisema lolote linawezekana kwa yeye kirejea Manchester
United siku moja na kwamba tusubiri kuona.
Mchezaji
wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo aliachana na penzi wake wa
zamani Irina Shayk baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka mitano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni