Timu ya taifa ya Al-geria leo wamelazimisha sare ya goli 2-2 na Taifa stars mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo kama ilivyoada kwa Waarabu wakiwa ugnini kucheza kwa tahadhari kubwa na kucheza mpira wa taratibu ndivyo ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza.
Wakati Al-geria wakicheza soka la taratibu Taifa stars walicheza soka la kasi na kusaka goli la kuongoza ambapo muda mwingi mpira waliutawala Stars na kuutengeneza nafasi kadhaa ambazo walishindwa kuzitumia.
Katika dakika ya 43 Elius Maguli akicheza mchezo wake wa kwanza chini ya kocha Mkwasa aliiandikia Stars goli la kwanza na kuipeleka Stars mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya kawaida huku Al-geria wakisaka goli la kusawazisha na katika dakika 49 walipata faulo nnje kidogo ya eneo la hatari ambapo mpigaji alipaisha mpira huo.
Dakika ya 54 Mbwana Ally Samata aliiandikia Stars goli la pili baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Algeria na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Algeria.
Kuingia kwa goli hilo kuliongeza umakini kwa Algeria na kujaribu kutafuta goli la ugenini huku Taifa Stars wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Algeria.
Katika dakika ya 62 Mbwana Ally Samata amanusura aipatie goli la tatu Taifa stars ambapo mpira wake uliamishwa mulekeo na beki wa LAlgeria.
Mkwasa alifanya Mabadiliko ya kumtoa Mudathir Yahya na Elius Maguli ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Said Khamisi Ndemla na Mrisho Ngassa.
Mabadiliko hayo yalitengeneza pengo katika eneo la kiungo ambapo Algeria walitumia vyema mwanya huo kupata magoli mawili ya haraka.
Katika dakika ya 71 Selmani Islam aliipatia goli la kwanza Algeria katika mazingira ambayo walinzi wa Taifa stars alidhani ameotea.
Katika dakika 75 pasi tatu toka kwa mlinda lango wa Algeria na mpira kuymkuta Selmani Islam katika eneo zuri na kumchamulia Ally Mustapha Bathez na kuizawadia Algeria goli la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Kama Stars wangekuwa makini leo wangekuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya goli 4, lakini wamrishi kufunga goli 2.
Matokeo ya sare ya magoli yanawaweka katika mahali pabaya Stars katika mchezo wa marejeano ambao utapigwa jumatano nchini Algeria.
Katika mchezo huo ujao Stars wanahitaji ushindi ama sare ya kuanzi goli 3 ili wafuzu kwa hatua inayo fuata.
Taifa stars leo: Ally Mustapha, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Himid Mao, Mudathir Yahya/Said Ndemla, Farid Mussa Maliki, Elius Maguli/Mrisho Ngasa, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni