STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 14 Novemba 2015

URUSI YAPIGWA MARUFUKU KUSHIRIKI RIADHA..........


Tokeo la picha la IAAF

Shirikisho la riadha la Urusi limeondolewa kwa muda kutoka kwa mashindano ya kimataifa, ikiwemo michezo ya Olimpiki, kwa tuhuma za kuhusika katika matumizi ya dawa za kutitimua misuli.

IAAF imechukua hatua hiyo baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya shirika la kukabiliana na dawa za kutitimua misuli duniani (Wada) iliyodai Urusi imekuwa “ikisaidia katika matumizi ya dawa za kuongeza nguvu misuli”.
 IAAF President Sebastian Coe addresses the media outside his office in London on Friday evening 
 Rais wa IAAF  Sebastian Coe akizungumza na vyombo vya habari.
 
Wanachama wa baraza la shirikisho hilo la riadha duniani walipiga kura 22-1 kuunga mkono Urusi ipigwe marufuku.

“Huu ni ujumbe muhimu sana kwetu,” rais wa IAAF Lord Coe amesema, na kuongeza kuwa amejitolea kufanikisha mabadiliko.
“Tunahitaji kujitafakari upya, kujichunguza sisi wenyewe katika mchezo huu, na tutafanya hilo.”

Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema marufuku hiyo ni ya “muda” na ni “tatizo linaloweza kutatuliwa”.

Mwakilishi wa taifa hilo katika baraza la IAAF hakuruhusiwa kushiriki kwenye kura hiyo iliyopigwa Ijumaa.

Mambo yalivyo kwa sasa, wanariadha wa Urusi hawawezi wakashiriki mashindano ya kimataifa ya riadha, ikiwemo msururu wa mashindano ya riadha duniani na michezo ya Olimpiki ya Rio itakayoanza Agosti mwaka ujao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari ameagiza uchunguzi ufanywe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox