KOCHA Mkuu wa Tanzania, Taifa Stars amewaanzisha pamoja washambuliaji Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Elias Maguri katika mchezo dhidi ya Algeria jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taifa Stars inamenyana na Mbweha wa Jangwani Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kuwania tiketi ya Kombe la Dunia Urusi 2018.
Na Mkwasa amerudi na ukuta ule ule maarufu wa Stars, ukiongozwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ mabeki Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati viungo watakuwa Himid Mao, Mudathir Yahya na Farid Mussa.
Katika benchi watakuwapo Aishi Manula, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salum Mbonde, Said Ndemla, Malimi Busungu, John Bocco na Simon Msuva.
Baada ya mchezo wa leo, timu hizo zitarudiana Jumanne mjini Algiers na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya mwisho ya mchujo, ambayo itachezwa kwa mtindo wa makundi.
Kikosi cha Taifa Stars leo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Himid Mao, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Elias Maguri na Farid Mussa.
Algeria inaweza kuwa hivi; Azzedine Doukha, Mohamed Khouti Ziti, Hichem Belkaroui, Carl Medjani, Yacine Brahimi, Ryad Boudebouz, Sofiane Feghouli, Walid Mesloub, Saphir Sliti Taider, Riyad Mahrez na Baghdad Bounedjah.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni