STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 19 Novemba 2015

USIYO YAJUA KUHUSU EL-CLASSICO...........




Real Madrid na Barcelona zitaumana kwenye mchezo wao wa ligi maarufu kama El Clasico utakaochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu Jumamosi ya November 21, katika historia ya mchezo huo Real Madrid maarufu kama Los Blancos wao ndio wanaongoza kushinda idadi ya mechi nyingi wakiwa wameshinda michezo 92 wakati Barelona wao wakiwa wameshinda mechi 89.

Kabla hujakaa chini kuangalia mchezo huo siku ya Jumamosi, inawezekana kuna baadhidi ya vitu ambavyo huvifahamu kuhusu mchezo huo mkubwa kwenye historia ya soka.

Ushindi mkubwa kwenyehistoria ya mchezo wa El Clasico
 
Real Madrid 11-1 Barcelona (13 June 1943)
Magoli Madrid vs Barca
Kwenye msimu wa mwaka 1943, Barcelona iliifunga Real Madrid magoli 3-0 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del Rey, lakini kikosi cha Real Madrid kilionesha kiwango kizuri kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka na kufanikiwa kuifunga Barcelona bao 11-1 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa marudiano na kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo.

         Kipindi kirefu bila kupoteza mchezo wa El Clasico
 
Barcelona: Mechi 13 (1 November 1917- 3 June 1928)
Madrid vs Barca 2Barcelona iliweza kucheza kwa miaka 11 bila kupoteza mchezo dhidi ya Real Madrid kwenye mashindano yote kuanzia November 1, 1917 hadi June 3, 1928, watoto wa Catalan pia wanashikilia rekodi ya kukaa muda mrefu zaidi bila kufungwa kwenye mchezo wa El Clasico kwenye ligi (La Liga) ikiwa hawajapoteza michezo saba, kuanzia December 2008 hadi December 2011 wakifanikiwa kushinda michezo sita kati ya saba.

Mfungaji bora wa muda wote kwenye El Clasico
 
Lionel Messi: Magoli 21
Madrid vs Barca 3Lionel Messi ndiye mcheaji anayeongoza kutupia kambani kwenye mechi ya El Clasico akiwa kafunga magoli 21 kwenye michezo 30 aliyocheza.

 Magoli 14 kwenye mechi za ligi (anafungana na Di Stefano), amefunga magoli matano kwenye michuano ya Super Cup na magoli mawili kwenye UEFA Champions League.

       Rekodi ya Kufunga mfululizo kwenye El Clasico
 
Madrid vs Barca 4

Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya mchezaji ambaye amefunga mfululizo kwenye mechi za El Clasio akiwa amefunga magoli 7 kwenye mechi 6 zilizopita tangu 2011-2012 Copa del Rey (mechi ya raundi ya kwanza) hadi 2012-13 mechi ya La Liga. 

           Nidhamu mbovu kwenye mechi za El Clasico
 
Madrid vs Barca 5
Mchezaji wa zamani na nahodha wa Real Madrid Fernando Hierro anaonekana kama mchezaji mwenye nidhambu mbovu kuwahi kutokea kwenye historia ya mechi za El Clasico akiwa amepewa jumla ya kadi 19 kwenye historia ya mchezo huo.

 Kati ya kadi hizo, 18 ni za njano huku moja ikiwa ni nyekundu.

Ramosi anaongoza kupewa kadi kwa wachezaji wa sasa, ameshaoneshwa kadi 16 (kadi 14 za njano na nyekundu mbili.


Ni mchezo unaowakutanisha wachezaji wenye rekodi ya kipekee Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, wote wanarekodi ya kuwa wachezaji pekee kuwa nominated katika kuwania tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka nane mfululizo, rekodi ambayo hakuna wachezaji waliowahi kuiweka, Messi ametwaa tuzo hiyo mara 4 na Ronaldo mara 3.
duo_3123946b
Ronaldo na Messi kila mmoja akiwa kashika tuzo yake ya Ballon d’Or

 Hii ndio itakuwa mechi ya El Clasico ya kwanza toka mwaka 1999 kuchezwa bila uwepo wa golikipa namba moja wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas aliyetimkia FC Porto ya Ureno na kukosekana kwa kiungo wa zamani wa FC Barcelona Xavi Hernandez.
28867
Casillas na Xaxi wakisalimiana katika moja kati ya mechi za El Clasico walizowahi kukutana.

Klabu ya Real Madrid ndio inaongoza kuifunga FC Barcelona mara nyingi, imeifunga jumla ya mechi 92 wakati FC Barcelona wameifunga Real Madrid mara 89.

Messi na Ronaldo ndio wachezaji wenye rekodi ya kipekee, kwani tofauti ya umri wao ni sawa na tofauti wa umri wa watoto wao. 

Ronaldo ni mkubwa kwa Messi yaani amemzidi Messi siku 869, ambapo ni utofauti wa mtoto wa Messi ambaye anaitwa na Thiago na utofauti wa mtoto wa Ronaldo anayeitwa Cristiano Ronaldo Junior ambapo yeye pia ni mkubwa kwa mtoto wa Messi kwa siku 869.
6057156223960338_20779271aa1c14ea9a0610f309660daf5c8c2c6a80e1f69f27ed706f81fe23ef_large

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox