Presha ya mechi za Ligi Kuu Uingereza
msimu wa 2015/2016 imefanya vilabu kadhaa kuanza kuingia katika mipango
ya kufanya usajili wa wachezaji licha ya kuwa dirisha dogo la usajili
bado halijafunguliwa. Klabu yenye presha kuliko zote ni klabu ya Chelsea ila klabu ya Manchester United ikiwa chini ya Louis van Gaal imeshaanza kuhusishwa na mastaa watano tofauti.
Kocha wa Man United Louis van Gaal ambaye anataka timu yake ifanye mashambulizi kwa kasi na kuongeza idadi ya magoli, Van Gaal ameongea kauli kuhusu mwenendo wa kikosi chake na kukiri kuwa bado kikosi chake hakina kasi anayoitaka na kuwatolea mifano Juan Mata na Jesse Lingard.
“Nilishazungumza
mara kadhaa katika mwaka wangu wa kwanza nikijiunga na Man United kuwa
nahitaji kikosi kicheze kwa kasi na ubunifu katika nafasi za winga,
umeona kwa sasa tunacheza na Jesse Lingard lakini sio miongoni mwa
mawinga wenye kasi zaidi duniani lakini pia Juan Mata” >>> Louis van Gaal
Hata hivyo stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk umetaja majina matano ya wachezaji ambao huenda wakasajiliwa na Man United, miongoni mwa majina hayo yanayotajwa kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili, majina yanayotajwa ni kusajiliwa na Van Gaal ni Sadio Mane kutoka Southampton, Riyad Mahrez kutoka Leicester, Alex Teixeira kutoka Shakhtar Donetsk, Karim Bellarabi kutoka Bayer Leverkusen na Felipe Anderson kutoka Lazio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni