
1- Mchezaji wa Mbeya City Juma Nyosso Kumdhalilisha nyota wa Azam FC John Bocco ni tukio baya la utovu wa nidhamu lililotokea katika Ligi Kuu Bara. Nyosso amefungiwa kucheza kwa muda wa miaka miwili.

2- Hirizi!...Mchezaji wa kimataifa wa Senegal, Papa N'daw aliyekuwa akikipiga Simba alizua tafrani baada ya kufumwa uwanjani akiwa na hirizi. Awali mchezaji huyo aliingia uwanjani dhidi ya Yanga akiwa na viatu vichakavu. Imani zake za kishirikina hazikumfikisha popote kwani mwisho wa yote Simba SC iliamua kumrejesha Senegal.

3- Watanzania wawili wanaokipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

4-Tanzania kulimwa bao 7-0 na Algeria katika mechi za awali kuwania kupangwa hatua ya Makundi kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi.
Kilikuwa ni kipigo cha kudhalilisha alichokipata kocha Charles Mkwasa na kikosi chake wakijalaumu kwa kupoteza nafasi nyingi mechi yao ya kwanza ya nyumbani.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni