Pamoja
na meneja wake, Jamal Kisongo kusema tayari Mbwana Samatta amesaini
mkataba wa awali wa miaka miwili na Genk, mshambuliaji huyo amesema bado
wanaendelea kuwasubiri TP Mazembe.
“Bado
tunasubiri Genk wamalizane na Mazembe, huwezi kumsainisha mchezaji wa
timu nyingine mkataba. Lakini mimi nimeshamalizana na Genk kwa maana ya
makuabaliano, suala la mkataba litafuatia,” alisema Samatta.
Samatta
anatarajia kuondoka nchini kwenda Nigeria katika tuzo za mchezaji bora
wa Afrika yeye akiwa anawania tuzo ya wachezaji wanaocheza ndani ya bara
la Afrika.
Samatta
anapewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kuisaidia TP Mazembe
kutwaa ubingwa wa Afrika pamoja na yeye kuibuka mfungaji bora.
Tamasha
maalum la tuzo hizo limepangwa kufanyika Januari 7 jijini Lagos,
Nigeria ikiwa ni siku mbili tu baada ya Samatta kutua nchini humo.
Wakati huohuo
Serikali imesema ipo bega kwa bega na mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwan Samatta kokote aendako.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemuambia Samatta
leo mbele ya waandishi wa habari kwamba Serikali itamuunga mkono kokote
aendako.
“Tuko
na wewe pamoja kokote uendako, pia ninakupongeza kwa kuwa sehemu ya
changamoto kwa wengine kutokana na mafanikio uliyofikia,” alisema Nape.
Samatta
ameishakubaliana na klabu ya Genk ya Ubeligiji na sasa limebaki suala
la Genk kumalizana na TP Mazembe ili Januari shughuli za uhamisho
zifanyike.
Samatta alitembelea ofisi za Waziri Nape na kusema alifika hapo kwa ajili ya kupata baraka kabla ya kwenda kokote.
“Nimekuja
kupata baraka, baraka za wazazi ni jambo muhimu sana kwa mtoto, ndiyo
maana nipo hapa,” alisema Samatta ambaye alielezea kuhusiana na mkataba
wa Genk.
“Suala
la kusaini bado, ila makubaliano yote yako safi. Nasubiri wao
wamalizane na TP Mazembe baada ya hapo mambo mengine yatafuatia,”
alisema Samatta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni