MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amepewa ya Pauni Milioni 75 kwenda kuungana na kocha Sven Goran Eriksson nchini China.
Ligi Kuu ya China inamtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United akawe nyota wao mpya, na ipo tayari kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 25 kwa msimu.
Hivyo kituo kipya cha kazi cha Rooney akiamua kuondoka Old Trafford — kinaweza kuwa Shanghai SIPG, ambayo iko chini ya kocha wa zamani wa England, Eriksson.
Wayne Rooney anatarajiwa kulipwa Pauni Milioni 25 kwa mwaka ili aondoke Manchester United kuhamia Ligi Kuu ya China
CSL, ambayo pia inamtaka Nahodha wa Chelsea, John Terry, inataka Rooney ambaye amebakiza Mkataba wa miaka mitatu Man United, ajiunge nao haraka iwezekanavyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni