CRYSTAL
Palace imemsajili Emanuel Adebayor aliyekuwa hana timu baada ya
Tottenham Hotspur kumtema na mara baada ya usajili huo alisema kuwa
anataka avunje rokodi ya Didier Drogba kuwa mwafrika aliye funga mabao
mengi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza.
Drogba amefunga mabao 104 na Adebayor yuko nyuma kwa mabao manane tu ili afikie rekodi hiyo.
Pia mshambuliaji huyo raia wa Togo aliyewahi kucheza Arsenal, Manchester City, Tottenham Hotspur na Real Madrid alisema ilikuwa inamuwia vigumu kukaa nje ya uwanja bila ya kucheza mechi za kimashindano.
Hata hivyo Adebayor alisema hata kama watu walikua hawamuoni akicheza ila alikuwa akiendelea kufanya mazoezi ya mpira katika kipindi hichi kigumu kwake. Ikumbukwe Adebayor amecheza dakika 17 tu tokea Januari 2015 .
Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa aliichagua Crystal Palace kwavile kuna marafiki zake pale na anapenda ligi kuu ya Uingereza ingawa zilikuwepo ofa nyingi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni