Gerard Pique ametajwa kuwa mwanamichezo bora wa
Catalan katika sherehe za 19 za Michezo za Catalan akiwatimulia vumbi
Andres Iniesta na Messi
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United amewapiku wapinzani wenzake akiwemo kiungo wa Barcelona Andreas Iniesta.
Beki huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 28 alikuwa na mchango mkubwa kwa timu yake kutwaa mataji matano 2015 ikiwa ni pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa.
Akipokea tuzo hiyo, Pique alisema: "Katika taaluma kuna nyakati mbaya na nzuri. Katika nyakati nzuri hupaswi kufikiri kwamba wewe unafanya vizuri kuliko yeyote mwingine na katika nyakati mbaya usifikiri kuwa unafanya vibaya kuliko wote. Kadiri miaka inavyokwenda utabaini kuwa unafuata njia yako mwenyewe."
Hali kadhalika Barcelona imetajwa kuwa timu bora ya Catalan katika hafla hiyo iliyofanyika katika makumbusho ya jiji hilo.
Pique alianza taaluma yake ya soka Nou Camp katika akademi maarufu
kama La Masia, lakini kabla ya kuingia kwenye timu ya wakubwa alijiunga
na Manchester United 2004.
Hata hivyo alipitia kipindi kigumu kwa kukosa namba kikosi cha kwanza akiwa Uingereza na Real Zaragoza alipocheza kwa mkopo, aliuzwa Barca miaka minne baadaye, mahali ambapo ameendelea na kuwa beki bora wa kati duniani.
Hata hivyo alipitia kipindi kigumu kwa kukosa namba kikosi cha kwanza akiwa Uingereza na Real Zaragoza alipocheza kwa mkopo, aliuzwa Barca miaka minne baadaye, mahali ambapo ameendelea na kuwa beki bora wa kati duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni