Mkali huyo wa miaka 30 amekuwa akisondwa kidole kwa
kusua-sua kiwango chake msimu huu, lakini amezijibu kelele hizo kwa
kutia kambani hat-trick dhidi ya Espanyol Jumapili.
Kabla ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Espanyol, supastaa huyo alikuwa ameshafunga mabao 16 katika mechi 21 alizocheza La Liga muhula huu - kazi nzuri kweli lakini bado alikuwa na mapungufu kulingana na kile mashabiki na wadau wa soka wamezoa kumwona akifanya dimbani.
Lakini Ronaldo alitia mpira kambani mara tatu kumfikia Luis Suarez katika chati ya upachikaji wa mabao Hispania, na amejiwekea historia zaidi ya mabao.
Katika mechi mbili walizokutana na Espanyol msimu huu, Mreno huyo amefunga mabao nane, kwa mara ya kwanza, hakuna mchezaji yeyote aliyefanikiwa kupata bahati hiyo kwa mpinzani mmoja kwenye kampeni za La Liga karne hii.
Moja ya bao lake lilipatikana ndani ya eneo la penalti - maana yake ni kwamba amefanikiwa kufunga kutoka yadi 12 msimu huu - mabao mengi katika eneo hilo kuliko mchezaji yeyote katika Ligi Kuu tano za Ulaya 2015-15.
Ameshinda penalti 14 katika ligi, tano zaidi kuliko mchezaji yeyote tangu 09-10.
Ronaldo pamoja na Karim Benzema na James Rodriguez kwenye orodha ya watikisa nyavu wana jumla ya mabao 64 ya ligi msimu huu. Hakuna klabu yoyote yenye mabao kama hayo katika Ligi za Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni