CHELSEA imemtaarifu beki wake wa muda mrefu, John Terry kwamba haitamuongezea mwishoni mwa msimu.
Nahodha huyo ametangaza ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya kuambiwa hataongezewa Mkataba.
Mkongwe huyo wa umri wa miaka 35 amethibitisha hayo baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya MK Dons katika mchezo wa Kombe la FA kutokana na kutopewa ofa ya Mkataba mpya Stamford Bridge.
Terry aliambiwa uamuzi huo wa klabu kwa simu kupitia kwa wakala wake kabla ya kuthibitishiwa ana kwa ana kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita, licha ya kukiri kwamba angependa kubaki Chelsea.
Nahodha wa Chelsea, John Terry ataondoka mwishoni mwa msimu Mkataba wake utakapomalizika
Mchezaji huyo wa muda mrefu zaidi wa klabu hiyo, amedumu Chelsea kwa miaka 21 na kushinda nayo mataji manne ya Ligi Kuu ya England, matano ya Kombe la FA, matatu ya Kombe la Ligi na mengine ya Ligi ya Mabingwa na Europa League.
Terry anataka kuendelea kucheza, lakini ameahidi hatasaini klabu nyingine ya England, huku akitarajiwa kwenda kumalizia soka yake China au Marekani.
"Hautakuwa mwisho wa kutendewa haki, sitastaafia Chelsea," amethibitisha Terry.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni