POLISI mmoja wa Dubai
anakabiliwa na kifungo cha miezi sita jela na faini ya euro 124,000 kwa
kutuma picha za video za pasi ya kusafiria ya mshambuliaji nyota wa
Barcelona Lionel Messi, katika mitandao ya kijamii.
Polisi huyo wa
Uwanja wa Ndege aliyejulikana kwa jina la J.J anatuhumiwa na waendesha
mashitaka kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano na alikiri kosa la kuvunja
Sheria ya Mtandao lakini aliomba kusamehewa.
Messi alitua Dubai mwishoni
mwa Desemba kuhudhuria sherehe za tuzo ya Globe Soccer ambao alishinda
tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na polisi huyo aliomba kama anaweza
kupiga picha na nyota huyo lakini ilishindikana kwasababu alikuwa
amechoka.
Polisi huyo mwenye umri wa miaka 26, baadae aliingia katika
chumba cha mawasiliano na kuirekodi video wakati Messi akionyesha pasi
yake ya kusafiria kwa wana usalama kabla ya kuituma katika mtandao wa
Snapchat.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni