GOLIKIPA wa Manchester
United David De Gea anaripotiwa kutaka kuendelea kubakia Old Trafford
hata kama Real Madrid watarejea kumuwinda tena mwezi huu.
Madrid
wanatarajiwa kukata rufani adhabu ya kufungiwa kusajili waliyopewa wiki
iliyopita lakini kama ikishindikana hawataweza kusajili mchezaji yeyote
mpaka kiangazi mwaka 2017.
Hata hivyo, bado wana uwezo wa kusajili
katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuna uwezekano wakaanza
tena kumfukuzia De Gea.
Usajili wa kipa huyo ulishindikana kidogo majira
ya kiangazi mwaka jana kutokana na karatasi muhimu kutowasili kwa
wakati.
De Gea ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka minne na United
anadaiwa kuwa kwasasa hatoweza kukubali tena kuondoka Old Trafford.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni