MSHAMBULIAJI nyota wa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa sasa wana mahusiano
mazuri na Lionel Messi na kutania kuwa bado anasubiri malipo yake kwa
kutoa huduma ya ukalimani wakati tuzo za Ballon d’ Or.
Wawili hao
wamekuwa mahasimu wakubwa katika tuzo hizo kwani katika kipindi cha
miaka nane iliyopita ni wao ndio wamezitawala.
Lakini akihojiwa mara
baada ya Madrid kushinda mabao 5-1 dhidi ya Sporting Gijon, nyota huyo
wa kimataifa wa Ureno amesisitiza kuwa kwasasa wana mahusiano mazuri na
nyota huyo wa Barcelona.
Ronaldo amesema wamekuwa karibu zaidi na
wamekuwa wakifurahia uhusiano wao mzuri kulinganisha na miaka ya
nyuma.
Messi na Ronaldo walipanda jukwaani pamoja ambamba na Neymar
katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or jijini Zurich na nyota huyo wa
zamani wa Manchester United mebainisha kuwa ilibidi awaokoe nyota hao wa
Barcelona.
Ronaldo amesema wakati wakiwa juu ya jukwaa sio Neymar wala
Messi ambaye anaweza kuzungumza kiingereza hivyo alibidi awe mkalimani
wao na kutani kuwa alizungumza nao baadae na kuwaomba wamlipe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni