Beki
wa kati wa Chelsea, Kurt Zouma ameumia goti lake upande wa nyuma baada
ya kutua vibaya wakati akirejea chini alipokuwa akiwania mpira wa juu
katika mechi dhidi ya Man United iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Beki huyo anaweza akakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu na tayari wachhezaji wengine wakianza wa Man United, wamekuwa wakimliwaza.
Juan
Mata, alimfuata palepale uwanjani na Marouane Fellaini alikuwa wa
kwanza kumpa pole baada ya mechi kwisha, lakini beki Luke Shaw ambaye
pia ni majeruhi pia alitupia mtandaoni akimuombea apone haraka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni