Kwa hivi sasa zipo taarifa ambazo zimezidi kusambaa kuwa kocha wa zamani wa Chelsea ,Mourinho atainoa klabu ya Manchester united baada ya kumalizika kwa msimu huu wa 2015-2016.
Sasa endapo Mourinho atatua na kuifundisha Manchester United mpinzani wake tangu alipokuwa nchini Uhispania alipokuwa anaifundisha Real Madrid, Pep Guardiola ambae atainoa Manchester City kwanzia msimu ujao, wawili hao watakutana mwezi wa saba mwaka huu tarehe 29 au 30 nchini China,Beijing au Shanghai katika mchezo wa maandalizi ya msimu wa 2016-2017.
Guardiola na Mourinho, Camp Nou kipindi Mourinho akiwa msaidizi wa Sir Bobby Robson's ,Guardiola akiwa ni mchezaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni