STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 20 Februari 2016

NI YANGA TENA... YAMUUA MNYAMA TAIFA, YAPAA KILELENI SIMBA PUNGUFU YASHUKA MPAKA NAFASI YA 3, AZAM KICHEKO MBEYA

Magoli ya Amis Tambwe na Donald Ngoma leo hii yamewamaliza Simba SC kwa goli 2-0, kartika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo wa leo ambao Simba SC kwa takribani dakika 66 walicheza wakiwa pungufu baada ya beki wake Abdi Banda kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 23 ya mchezo ikiwa ni baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano

Yanga sc waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza kama mpigaji wa faulo angeipiga vyema yanga wangeandika goli la kwanza lakini mpira wake uliishia mikononi mwa kipa Vicent Agban.

Baada ya kosa kosa hiyo Simba SC nao walijibu pigo na kuendelea kushambuliana kwa zamu kwa dakika 23 za mwanzo kabla ya Banda kupewa kadi nyekundu.

Yanga SC waliandika goli la kwanza katika dakika ya 39 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye aliwahi mpira ambao Hassan Kessi aliurejesha kwa kipa na mpira kuwa mfupi na kupelekea Ngoma kumchambua kipa na kuiandikia Yanga goli la uongozi.

Goli hilo lilpeleka Yanga kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, na katika kipindi cha pili Simba SC walijaribu kusaka goli la kusawazisha bila mafanikio.

Katika dakika ya 71 Amisi Tambwe akiungfa krosi ya mtokea benchi Geofrey Mwashiuya na kuiandikia yanga goli la pili, goli lililo imaliza Simba SC na kupelekea kupoteza mchezo kwa kukubali kufungwa goli 2-0 na yanga.

Ushindi huo wa pili msimu huu Yanga SC wanaupata mbele ya Simba SC unaifanya Simba SC kushuka mpaka nafasi ya tatu huku Yanga ikirejea kilelelni na Azam FC wakishika nafasi ya pili.


Kwa upande wa Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ambaye amefunga bao la pili katika mechi ya leo ambapo Yanga imeilaza Simba kwa mabao 2-0.



Beki Abdi Banda alilambwa kadi ya njano ya pili katika dakika ya 25 na kuzaa nyekundu baada ya kumwangusha Donald Ngoma.



Tambwe alifunga bao katika dakika ya 72 baada ya beki Juuko Murshid kushindwa kumdhibiti baada ya krosi safi ya Geofrey Mwashiuya.



“Tulianza vizuri, mechi ilikuwa na ushindani mkubwa. Lakini baada ya ile kadi nyekundu, ilitusaidia sisi kuingia kwa wingi katikati na kuwabana Simba.



“Mechi ilikuwa nina ushindani sana, Simba walijitahidi kucheza vizuri licha ya kuwa pungufu. Lakini sisi tulikuwa bora zaidi leo,” alisema Tambwe raia wa Burundi.




Hilo ni bao la 15 msimu huu, huku akiwa amebakiza bao moja tu kumkamata Amissi Kiiza ambaye ana mabao 16.
Na kule jijini Mbeya
Mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC wameendeleza wimbi lao la ushindi mbele ya Mbeya city katika uwanja wa Sokoine baada ya leo kuifunga goli 3-0 na kusogea hadi nafasi ya 3.

Katika mchezo huo ulioharibiwa na mvua ulianza kwa kasi huku kila timu ikishambuliana kwa zamu kabla ya mvua kuanza kunywesha na kuwafanya wachezaji wa Mbeya city kuteleza mara kwa mara.
Katika dakika ya 41 Kipre Herman Tcheche aliiandikia Azam FC goli la kwanza akiunga kona na Himidi Mao Mkami na kuipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Azam FC wakiingia na jezi tofauti na zile zilizopigwa na mvua kipindi cha kwanza, walikianza kwa kujiami kwanza huku Mbeya city wakirejea kwa kasi, ambayo kila dakika ilivyokuwa inasogea Mbeya city kasi yao ilikuwa ina pungua.

Katika dakika ya 63 John Bocco anaumalizia mpira uliomshindwa Juma Kaseja baada ya kuteleza na kuiandikia Azam FC goli la pili ambapo lilipeleka Azam Fc kuutawala mchezo.

Mpira uliomgonga kwenye goti Kaseja wakati anajiandaa kudaka unamkuta Farid Mussa Maliki na kuiandika Azam FC  goli la 3 na kupeleka mchezo kumalizika kwa Azam Fc kuibuka na ushindi wa goli 3-0.

Ushindi huo unaifanya Azam Fc kufikisha pointi 45 ambazo zinawawaweka katika nafasi ya pili na kuishusha simba sc hadi nafasi ya 3 kwa uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa. 
  Mechi za leo 2016-02-20
FTYANGA 2 : 0SIMBA SC
FTMGAMBO JKT 1 : 1T.PRISONS
FTSTAND UNITED 1 : 1JKT RUVU
FTMBEYA CITY 0 : 3Azam FC
FTTOTO AFRICANS 1 : 1KAGERA SUGAR
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox