Jumapili ya February 28 Ligi Kuu
Ubelgiji iliendelea tena kwa klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania
Mbwana Samatta kushuka katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena
kucheza mchezo wake wa 28 wa Ligi Kuu dhidi ya vinara wa Ligi Club
Brugge.
Licha ya kuwa Club Brugge walikuwa
wanarekodi nzuri dhidi ya Genk wamekubali kipigo cha goli 3-2, kwani
kabla ya mchezo huo, Genk na Brugge kwa mechi tano zilizopita, Brugge
walikuwa wameifunga Genk mara tatu, sare moja na kupoteza mechi moja.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na
Nikolaos Karelis dakika ya 31, ikiwa ni dakika 21 zimepita toka Club
Brugge wapate goli la kuongoza dakika ya 15 kupitia kwa Thomas Meunier,
lakini kasi ya Genk iliongezeka na kupata goli la pili dakika ya 50
kupitia kwa Thomas Buffel.
VIDEO YA GOLI
Mbwana Samatta aliingia dakika ya 79
kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis aliyefunga goli la kwanza la KRC
Genk. mabadiliko ya kuingia Mbwana Samatta yalikuwa na faida kwani,
dakika 2 baada ya kuingia alipachika goli lake la kwanza akiwa na Genk
lakini pia ni goli la tatu kwa Genk, kabla ya dakika ya 83 Brugge
walifanikiwa kupata goli la pili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni