Timu ya Manchester United iko mbioni
kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kuwa klabu ya kwanza kabisa kuvuna
mapato ya zaidi ya pauni nusu bilioni kwa mwaka mmoja.
Mapato kwa robo ya pili ya mwaka yamepanda na kufikia pauni milioni 133.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.6 kutoka ya mwaka uliopita wa fedha.
Mapato kutokana na matangazo yamepanda kwa asilimia 31.3 na yale ya udhamini kwa robo ya pili ya mwaka yamepanda kwa pauni milioni 1.6 na kufikia pauni milioni 37.4.
Pia, Man United sasa wapo kwenye uvumi mkubwa kuwa meneja wao, Louis van Gaal, atabadilishwa mwishoni mwa Msimu na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
SUNDERLAND
Klabu ya Sunderland imefuta Mkataba
na Mchezaji wake Adam Johnson mara tu baada ya mchezaji huyo kukiri
Makosa Mawili Mahakamani kwenye Kesi iliyomkabili ya kuwa na uhusiano wa
ngono na Binti wa chini ya Miaka 16.
Meneja wa Sunderland, Sam Allardyce, alithibitisha kuwa Johnson hatakuwemo kwenye Kikosi cha Timu yao ambacho Jumamosi kitacheza na Manchester United.
Mkataba wa winga huyu umevunjwa mara tu baada ya Kampuni ya Kutengeneza Vifaa vya Michezo, Adidas, kuamua kuvunja Mkataba wa Udhamini na Mchezaji huyo.
Kesi ya Johnson itaendelea Bradford Crown Court Ijumaa ambako anakabiliwa na Jumla ya Mashitaka Manne ambayo yote awali aliyakana.
Kwa makosa ambayo ameyakiri, Mchezaji huyo sasa ana hatari ya kufungwa si zaidi ya Miaka Miwili na Nusu.
Johnson, alizaliwa mjini Sunderland alianza kucheza soka katika timu ya Middlesbrough kisha akajiunga na Manchester City kabla ya kusajiliwa na Sunderland, kwa dau la pauni milioni 10 mwaka 2012.
WEST HAM UNITED
Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya West ham, Dimitri Payet amesani mkataba mpya wa miaka mitano na timu yake.
Mapema wiki hii klabu yake ilizikataa taarifa zilizosambaa kuwa mchezaji huyo anataka mkataba mpya, huku mkataba wake wa kwanza pia ukiwa ni miaka mitano.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Ufaransa amezifumania nyavu mara 6 katika michezo 22 aliyocheza na kuiweka West Ham katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu ya England.
David Sullivan, mmiliki wa timu hiyo amesema "tutafanya chochote kuwabakiwa wachezaji wetu wazuri na Payet ni mchezaji mzuri."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni