TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.
KLABU ya Manchester
United inajipanga kutoa ofa ya paundi milioni 35 kwa ajili ya kumuwania
Nicolas Gaitain, ingawa Atletico Madrid na Zenit St Petersburg nazo pia
zinamuwinda winga huyo wa Benfica.
Chanzo: Record
MSHAMBULIAJI wa Bayer Leverkusen Javier Hernandez anajipanga kujiunga na Arsenal mwishoni mwa msimu wa 2015-2016. Pamoja na klabu hiyo kukataa kumuuza kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari lakini Arsenal wao wana uhakika wa kumnsa majira ya kiangazi.
Chanzo: Liverpool Echo
KLABU ya Tottenham Hotspurs ilituma maskauti wake kwenda kushuhudia ushindi wa Mainz dhidi ya Hannover mwishoni mwa wiki iliyopita. Spurs walifanya hivyo kutokana na nia yao ya kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uturuki Yunus Malli.
Chanzo: Tuttomercatoweb.com
KLABU ya Orlando City iko katika mazungumzo na D.C. United ili kupata haki za MLS kwa ajili ya kiungo wa AC Milan Antonio Nocerino ambaye anategemewa baadae kusajiliwa Florida. United ndio waliokuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na Nocerino lakini yalivunjika.
Chanzo: Washington Post
KLABU za Manchester City na Manchester United zinatarajiwa kupambana kumfukuzia Neymar majira ya kiangazi ambapo klabu zote mbili zinaripotiwa zitakuwa tayari kumlipa nyota huyo wa Barcelona mshahara wa paundi milioni moja kwa wiki.
Chanzo: The Sun

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni